1. Kwanza Anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Kiasi cha Tsh. 640,000,000/= (Milioni Mia Sita Arobaini) ikiwa ni mgao wa fedha za ruzuku ya miradi ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2025/2026 ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
2. Hivyo anawatangazia wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuwa Halmashauri imepokea jumla ya Shilingi 640,000,000/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali yaliyoorodheshwa katika kiambatisho hapa BARUA MAPOKEZI YA FEDHA ZA RUZUKU NA MIRADI YA MAENDELEO KUTOKA SERIKALI KUU.pdf
3.Fedha hizo zilizopokelewa ni asilimia miamoja (100%) ya fedha za ruzuku ya miradi kutoka Serikali Kuu zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2025 - 2026
4. Fedha hizi zilizotolewa na Serikali Kuu ni katika muendelezo wa Juhudi za kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Ludewa
EWE MWANANCHI SHIRIKI KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU TAREHE 29-10-2025.
KUMBUKA KUPIGA KURA NI HAKI YAKO.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.