Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa POLIO nchini Malawi, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa itaanza zoezi la kampeni ya utoaji wa chanjo ya matone ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5).
Chanjo itaanza kutolewa kuanzia tarehe 27 Machi 2022, saa 1:30 asubuhi katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, pia timu ya watalamu na wahamasishaji watapita nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuhamasisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano (5) wapate chanjo.
Aidha katika kampeni hii watoto wote ambao walichanja na wale ambao hawakuchanja chanjo ya matone ya POLIO watapatiwa chanjo ili kuwakinga na mlipuko wa POLIO ulio tangazwa nchini Malawi.
Chanjo ya matone ya POLIO inasaidia kuimarisha kinga ya mtoto dhidi ya maambukizi na madhara ya ugonjwa wa POLIO ambao ni ulemavu wa viungo na vifo kwa watoto.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, anatoa wito kwa wazazi/walezi wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano (5) wahakikishe wanawafikisha watoto hao kwenye vituo vya afya ili wapatiwe chanjo ya POLIO.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.