Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomas amekabidhiwa rasmi Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Makete Kissa Gwakisa. Ambapo Mwenge huo wilayani Ludewa unakimbizwa KM. 92.2 na kupita katika vijiji kumi (10) na kata sita (6) za halmashauri hiyo, huku miradi sita (6) yenye jumla ya thamani ya Tsh. 3, 094, 330,019. 00 ikiangaziwa na mwenge huo.
Mbio hizo za Mwenge Kitaifa zikiongozwa na mkimbiza Mwenge Ismail Ali Ussi zinapita katika mradi mradi wa Ujenzi wa nyumba ya kulala wageni wenye thamani ya Tsh. 334,324,000.00, Ujenzi wa shule ya Sekondari ya Amali ya Mkoa wa Njombe thamani ya Tsh. 1,623,618,000.00, Ujenzi wa mradi wa maji Mavala wenye thamani ya Tsh. 1,070,692019.00, Mradi wa huduma endelevu za maji na usafi wa Mazingira (WASH) wenye thamani Tsh. 50,980,000.00 pamoja na mradi wa Mradi wa Kilimo cha mahindi wa kikundi cha vijana cha SISI kwa SISI wenye thamani ya Tsh. 14,716,000.00.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.