Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dkt. Selemani Jafo, ameiambia jamii ya Watanzania kwamba mradi wa Liganga na Mchuchuma utaanzishwa hivi karibuni, na kwamba utakuwa na manufaa makubwa kwa uchumi wa taifa. Akizungumza wakati wa ziara yake katika mkoa wa Njombe, Mh. Jafo alisisitiza kuwa serikali iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo muhimu, ambao utachochea maendeleo katika sekta ya viwanda na kuongeza ajira kwa wananchi.
Mh. Jafo alisema kuwa, mradi wa Liganga ni mojawapo ya miradi mikubwa ya kimkakati ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hususani kupitia uzalishaji wa chuma, ambacho ni malighafi muhimu katika viwanda mbalimbali. Alieleza kuwa, kuanzishwa kwa mradi huo kutaleta mageuzi katika sekta ya madini, ambapo Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi zitakazozalisha na kutumia chuma kwa ajili ya viwanda vyake.
"Mradi wa Liganga na mchuchuma utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa letu. Tunasimamia kwa karibu hatua zote za utekelezaji na tutahakikisha kuwa mradi huu unawanufaisha wananchi na kuchangia ukuaji wa viwanda na ajira," alisema Mh. Jafo.
Aidha,Mbunge wa jambo la Ludewa, Mh. Joseph Kamonga, ameiomba serikali kupitia Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dkt. Selemani Jafo, kujenga kituo cha kupoozea umeme katika wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe. Ombi hili linatokana na hitaji la kupata umeme wa kutosha kwa ajili ya kuendesha viwanda vikubwa na kuchochea maendeleo ya viwanda katika mkoa wa Njombe.
Akizungumza wakati wa ziara ya Mh. Jafo katika wilaya ya Ludewa, Mh. Kamonga alisema kuwa, uwepo wa kituo cha kupoozea umeme utasaidia katika upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika, jambo litakalowawezesha wananchi na wawekezaji kuanzisha na kuendeleza viwanda vikubwa katika wilaya hiyo. Alisisitiza kuwa, umeme wa kutosha ni muhimu katika kufanikisha malengo ya serikali ya kuendeleza sekta ya viwanda na kuimarisha uchumi wa taifa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.