Katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olivanus Thomas, ameungana na wananchi wa Ludewa Mjini leo tarehe 5 Juni 2025 kushiriki shughuli za usafi wa mazingira kwa kuokota taka za plastiki na nyinginezo zilizokuwa zimezagaa maeneo mbalimbali ya mji huo, kwa lengo la kuhakikisha mji unakuwa safi na salama kwa afya ya jamii.
Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano maalum kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya (Bomani) na kupitia maeneo tofauti ya mji wa Ludewa, yakiwemo viwanja vya Halmashauri, stendi ya zamani ya magari, mitaa mbalimbali, na maeneo ya ofisi za wafanyabiashara.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo la usafi, Mheshimiwa Thomas aliwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushiriki, na kuwataka kuendeleza tabia ya kufanya usafi mara kwa mara badala ya kusubiri maadhimisho pekee. Alisisitiza kuwa mazingira safi yanachangia afya njema na maendeleo ya jamii.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ludewa ndg. Castory Kibasa aliwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushiriki zoezi hilo la usafi, na alisema kauli mbiu ya mazingira 2025 "Mazingira yetu na Tanzania ijayo tuwajibike sasa, Dhibiti matumizi ya plastiki".
Wananchi na wafanyabiashara kutoka maeneo tofauti ya Ludewa walijitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo, hali iliyosaidia kufanikisha tukio hilo kwa mafanikio makubwa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.