Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mnamo Januari 17, 2023 alifanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Njombe na kutembelea maghala mbalimbali ya pembejeo za Kilimo.
Mhe. Waziri aliagiza kufungiwa kibali kwa kampuni ya Kandia Fresh pamoja na kutojihusisha na ununuzi na uuzaji wa matunda ya Parachichi ndani na nje ya nchi kutokana na kampuni hiyo kununua Parachichi ambazo hazijakomaa kisha kuzitupa dampo.
Mhe. Bashe alitoa agizo hilo jana mara baada ya kusambaa kwa video iliyoonesha rundo la Parachichi zikiwa zimetupwa mjini njombe.
Waziri Bashe alisema ni marufuku kuchuma Parachichi ambazo hazijakomaa kwa sababu hakuna soko kwa aina hiyo ya parachichi bali ni kuharibu soko la parachichi kimataifa.
Aidha alisema wizara imeandaa muongozo utakaotumika kitaifa kusimamia mnyororo mzima wa uzalishaji wa zao la parachichi.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Waziri wa Kilimo amewaagiza mawakala wa mbolea Mkoa wa Njombe EGT kufungua tawi Wilayani Ludewa ili kukabiliana na changamoto ya wakulima kusafiri umbali mrefu kufuata mbolea.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka walimpokea Mhe. Waziri wa Kilimo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga alimshukuru Mhe. Waziri wa Kilimo kwa kuona umuhimu wa kufungua tawi la upatikanaji wa mbolea Wilayani Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.