RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEMTEUA BWANA CHARLES EDWARD KICHERE KUWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG):
Bwana Charles Edward Kichere aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, anachukua nafasi ya Prof. Musa Assad Aliyemaliza muda wake kwa mujibu wa Sheria, Novemba 4, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Bwana Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kuchukua nafasi ya Profesa Musa Assad aliyemaliza muda wake kwa mujibu wa Sheria Novemba 4, 2019. Katika Taarifa yake kwa umma, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Ndugu Gerson Msigwa amesema kwamba Mheshimiwa Rais amefanya uteuzi huo leo Novemba 3, 2019 na kwamba pamoja na wateuliwa wengine wataapishwa kesho Novemba 4, 2019 kuanzia saa 3.30 asubuhi Ikulu Jijini Dar Es Salaam. Katika uteuzi wa leo, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia amewateua Majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.