Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imeibuka kidedea katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kufuatia kuhitimisha Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2019 kwa miradi yake yote kupitishwa na Mwenge wa Uhuru. Hayo yamejiri baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili, kukagua miradi miwili, na kuzindua miradi mitatu kati ya miradi saba ya Wilaya ya Ludewa. Akizungumza wakati wa kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Lugarawa, Ndg. Mzee Mkongea Ali alinukuliwa akisema kwamba ujenzi wa zahanati hiyo, pamoja na kujuimuisha asilimia kubwa ya ujenzi huo kwa nguvu za wananchi, lakini imejengwa kwa viwango bora kabisa kiasi ambacho Mbio za Mwenge kwa mwaka 2019 zimeridhia kuweka jiwe la msingi. Aidha alinukuliwa akisema kwamba kwa namna wananchi wa kijiji hicho walivyojitoa kwa juhudi, angependa sana naye kuwa sehemu ya wakazi wa kijiji hicho. "Mmefanya kazi nzuri sana, kiasi kwamba nami natamani ningekuwa nimezaliwa hapa" alinukuliwa akisema Kiongozi huyo. Mradi mwingine uliosifika sana na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 ni ule wa ujenzi wa tenki kubwa la maji katika Kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga. Akiweka jiwe la msingi, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesema, mpaka wa kati wa kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa maji, ulikuwa ndio mradi Bora kabisa katika miradi yote iliyokuwa imetembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu. Ikumbukwe ni mikoa mitatau tu ilikuwa imesalia mpaka akiweka jiwe la msingi la mradi huu wa Kijiji cha Mbugani Wilayani Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.