Chrispin Kalinga - Ludewa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, amefanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Njombe ambapo alianza ziara yake tarehe 26 Oktoba 2023 na amehitimisha leo tarehe 28 Oktoba 2023 katika Uwanjwa wa Mpira wa Miguu CCM Mkoa wa Njombe.
Dkt. Mpango, amefanya ziara katika Wilaya ya Wanging'ombe, Wilaya ya Makete na amemaliza ziara yake leo katika Wilaya ya Njombe.
Kote huko amekagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliopo Kijiji cha Masisiwe wilayani Makete, ameweka jiwe la msingi mradi wa maji lugenge, ameweka Jiwe la Msingi katika Kiwanda cha MSD cha kutengeneza Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi Makambako,
ametembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda cha Uchambuzi na Ufungashaji Parachichi cha AvoAfrica kilichopo Makambako, ametembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda cha uchakataji wa bidhaa za mbao cha Tanganyika Wattle (TANWAT) kilichopo Kibena na leo Oktoba 28, 2023 Mhe. Dkt. Philip Mpango amekagua bidhaa wakati akitembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Nne ya SIDO Kitaifa yanayoendelea Hadi tarehe 31 Oktoba katika uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.
Aidha, wakati akikagua mabanda mbalimba kwenye maonesho 4 ya SIDO Kitaifa Mkoani Njombe Mhe. Dkt. Philip Mpango amempongeza mbunifu wa kinu cha kuyeyusha chuma cha Liganga Bw. Reuben Mtitu anayetokea Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Pia Mhe. Philip Mpango ameweka Saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini - Njombe Mchungaji Dkt. Gabriel Nduye na amemfariji Askofu wa Kanisa KKKT Dayosisi ya Kusini - Njombe Dkt. George Fihavango kufuatia kifo cha msaidizi wake mchungaji Dkt. Gabriel Nduye wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Mheshimiwa Philip Mpango alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. @anthony_mtaka
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.