Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ludewa Bi. Clementina Kabaka anawatangazia Wakulima na Wananchi wote wenye mashamba yanayolimwa Ndani ya Wilaya ya Ludewa,wamiliki wa mashamba na waliokodi,watu binafsi,vikundi na vyama vya Ushirika vyenye mashamba ya pamoja,kampuni,Taasisi na yeyote anayejihusisha na kilimo cha zao lolote .
Wanatangaziwa kufika ofisi za kijiji shamba lilipo ili kujisajili kwa ajili ya kupata mbolea za ruzuku.wataalamu wa ugani na watendaji wa maeneo husika watakuwepo kusimamia zoezi zima .zoezi hili litafanyika awamu mbili
Awamu ya kwanza ni kutoa taarifa binafsi na taarifa za shamba na mazao
Awamu ya pili ni kupiga picha,kuchukua alama za vidole na kupata alama ya utambulisho itakayotumika wakati wa kununua mbolea.
Zoezi la usajili litafanyika ndani ya siku 10 tu zoezi limeanza 12/8/2022 hadi 22/10/2022.
Nenda na kitambulisho cha NIDA/Mpiga kura ,leseni ya udereva au passport .kwa maelezo zaidi wasiliana na mtendaji wa kijiji lilipo shamba lako.kama una mashamba maeneo tofauti jisajili sehemu zote.unaweza kuwasiliana pia na Afisa kilimo Wilaya 0768825570/0620243683.
#JiandaeKuhesabiwa
#23/08/2022
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.