Wilaya ya Ludewa Katika Maandalizi Kabambe ya Kuupokea Mwenge wa Uhuru. Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ipo kwenye maandalizi kabambe ya kuupokea Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kufika Wilayani hapo mnamo Tarehe 20-09-2019. Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika Kata ya Lupanga Kijiji cha Lusala ukitokea katika Wilaya ya Makete. Unatarajia kuzindua Miradi Kadhaa ya Kimaendeleo kama Vile Shule na Zahanati. Pia utakagua mradi wa umeme wa maji unaotarajiwa kuzinduliwa mapema mwaka huu 2019. Katika kufanikisha zoezi hili, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya imeweka mikakati kabambe ikiwemo kutembelea na kukagua mara kwa mara shughuli zitakazopitiwa na Mwenge ili kuhakikisha fedha zinazotumika kujenga miradi hiyo zinakuwa na thamani halisi ya fedha za wananchi (Value for money). Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo pia amewaagiza Wakuu wa Idara na Vitengo kuhakikisha shughuli zote hazikwami ili wananchi wapate huduma zilizokusudiwa na Serikali katika kuanzisha na kutekeleza miradi hiyo. Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 Wilayani Ludewa utahitimisha ziara kwa mkesha utakaofanyika katika Kata ya Mavanga. Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mheshimiwa Andrea Tsere amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru ili waweze kujipatia Elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge na Wakimbiza Mwenge kuhusu masuala mbalimbali kama vile umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji, na kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu mwezi Novemba.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.