Mradi unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa Ufadhiri wa Serikali Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Umetengewa Fedha Taslimu Kiasi cha Shilingi za Kitanzania Milioni Mia Nne. (Tsh. 400,000,000/=) mpaka kukamilika kwake.
Unatekelezwa kwa kutumia wataalamu wa ndani ambapo kunajengwa miundombinu ifuatayo;
1 Ujenzi wa Nyumba ya Kuishi Mtaalamu (Daktari).
2.Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto (Wodi ya Kina Mama)
3.Maabara kwa ajili ya vipimo mbalimbali vya Afya.
4.Chumba cha Upasuaji (Theater)
5.Chumba cha Kuhifadhi Maiti (Motuary)
Mradi umepangwa kukamilika katika muda wa majuma kumi na sita. Kukamilika kwake kunatarajiwa kuwa suluhu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wakazi wa Wilaya ya Ludewa, hususani wale wanaotokea katika tarafa za Masasi na Mwambao, kwani panatarajiwa kuwa na maboresho makubwa sana katika sekta ya afya katika Wilaya yetu.
Hii vile vile ni Neema katika Wilaya yetu kwani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi inatarajia Kujenga Meli Kubwa ya Abiria katika Ziwa Nyaza, hivyo kurahisisha huduma za usafiri katika Tarafa ya Mwambao, ambapo wakazi wa huko itakuwa ni rahisi kufikia huduma za Afya katika Kituo chao bora kabisa cha manda baada ya kukamilika kwa Ujenzi wa Uboreshaji Miundombinu hiyo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.