Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Februari 04, 2023 alifanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Ludewa na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na wakala wa misitu na Maliasili.
Pamoja na mambo mengine, alizindua zoezi la upandaji miti katika wilaya ya Ludewa na kushiriki zoezi la upandaji miti zaidi ya 300 ambayo ilipandwa katika eneo la shule ya sekondari Ludewa. Pia ametembelea bweni linalojengwa katika shule ya sekondari Ludewa Kwanza ambayo ni Shule Teule.
Aidha, Mhe. Waziri Balozi Pindi Chana alikabidhi gari moja lenye thamani ya shilingi milioni 170 litakalotumika katika shughuli mbalimbali za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilayani Ludewa.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina. Pia walikuwepo Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Ludewa wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndg. Stanley Kolimba , Wakuu wa divisheni na vitengo wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert Ngailo.
Wakati akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Ludewa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mheshimiwa Waziri alipokea zawadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa umoja wa wanaweke wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ludewa. Zawadi hiyo ilitolewa kama alama ya shukrani kwa Mheshimiwa raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyochapa kazi na kuipa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.