unge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga ananendelea na ziara ya kutembelea kijiji kwa kijiji ndani ya Wilaya ya Ludewa.
Mhe. Mbunge aliaanza rasmi ziara yake Julai 7, 2023 ambapo mpaka sasa amefanikiwa kuzifikia kata 10 kati ya 26 na vijiji 29 kati ya 77.
Malengo na Matamanio ya Mhe. Mbunge ni kuhakikisha anazifikia kata zote 26 na vijiji vyake 77 kwa lengo la kupeleka mrejesho wa yale waliyo mtuma akayawasilishe Bungeni , kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020 - 2025. na kusikiliza kero za wananchi kwaajili ya kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wa kata mpaka jana Julai 23, 2023 Mhe. Mbunge amefanikiwa kuzifikia kata zifuatazo ambaoo leo ataendelea na kata ya Mkongobaki
1. Madilu
2. Madope
3. Lubonde
4. Lupanga
5. Mlangali
6. Iwela
7. Mundindi
8. Mavanga
9. Nkomang’ombe
10. Lugarawa
Na kwa upande wa vijiji, Mhe. Mbunge amefanikiwa kuvifikia vijiji vifuatavyo na kufanya mikutano ya hadhara.
1. Ilininda
2. Ilawa
3. Mfalasi
4. Manga
5. Madilu
6. Mangalanyene
7. Madope
8. Luvuyo
9. Mkiu
10. Masimbwe
11. Kiyombo
12. Ligumbiro
13. Lufumbu
14. Mlangali
15. Itundu
16. Kimelembe
17. Nkomang’ombe
18. Iwela
19. Amani
20. Mundindi
21. Njelela
22. Mavanga
23. Mbugani
24. Lupanga
25. Lusala
26. Utilili
27. Shaurimoyo
28. Mdilidili
29. Lugarawa.
Mhe. Mbunge anatoa shukrani za dhati kwa wale wote walio shiriki na wanaoendelea kushirki kufanikisha ziara hii kuanzia Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ndani ya Wilaya ya Ludewa, Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote alizo fanya ziara, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya bila kuwa sahahu wananchi ambao walijitokeza kwa uwingi kumpokea na kumsikiliza
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.