Jana Februari 23, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Daniel Ngalupela pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa pamoja na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ludewa na kufanya kikao kazi na wananchi wa Kata ya Lugarawa juu ya majanga ya moto yaliyotokea Februari 14 na 21, 2023 katika mabweni ya Shule ya Sekondari Lugarawa.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amepokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati wa bweni la wanafunzi wa kiume shuleni hapo; baada ya Ushirikiano baina Ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mbunge wa Jimbo la Ludewa na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kidini na wananchi waliojitolea na kukarabati Bweni Baada ya ajali ya moto kutokea tarehe 14 Februari 2023.
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya amepokea taarifa za jaribio la kuchoma bweni la watoto wa kike lililofanyika Februari 21, 2023 na kupelekea kuungua kwa magodoro matatu, shuka na blanketi lakini uharibifu wa miundombinu uliotokea katika harakati za kuuzima huo moto.
Mkuu wa Wilaya ameelekeza Idara ya zima moto Wilaya kutoa Elimu mashuleni na kwa wananchi juu ya namna ya kupambana na majanga ya moto.
Amewaomba Wananchi na wanafunzi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama, sambamba na kamati iliyoundwa kuchunguza majanga hayo ili kubaini vyanzo vya moto na wahusika kutokana na ushaidi na viashiria husika.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewaasa wanafunzi kuongeza juhudi katika masomo yao ili wanendelee kufanya vyema ngazi ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan- ameonesha dhamira ya kuendelea kuboresha Taaluma nchini- kwa Kuongeza Bajeti za miundombinu ya Elimu hivyo ni wajibu wa wananchi kutunza miundombinu hiyo kwani ni uwekezaji Wenye manufaa kwa jamii.
Mkutano huu wa umma ulitoa nafasi ya wananchi kuwasikiliza viongozi wa ngazi mbalimbali na kwa umuhimu zaidi kutoa maoni yao, ushauri wao katika kustawisha Taaluma na maendeleo ya jamii kiujumla.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.