Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkomang'ombe Wilayani Ludewa Bi. Tumaini Ng'ande amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi mbalimbali kwenye Kata hiyo ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi mbalimbali za Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 Kwa kulipa fidia wananchi ya Kata hiyo na maeneo mengine ya jirani huku Kata hiyo ikiwa imenufaika na zaidi ya Bilioni 4 walizolipwa wananchi ili kupisha Mradi ya Makaa ya mawe.
Aliyasema hayo alipotembelewa na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Chrispin Kalinga alipokuwa wakitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Kata hiyo Jana Novemba 08, 2023.
"Kata ya Nkomang'ombe imepokea fedha za kutekeleza miradi mbalimbali na miradi hiyo imekamilika ikiwa ni pamoja na Zahanati ya Kimelembe iliyogharibu hadi kukamilika kwake kiasi cha shilingi milioni 50, Upunguzwaji wa Milima kimelembe zaidi ya Bilioni 4 zimeletwa hapa na Mkandarasi yupo anaendelea na kazi, tulipokea Bilioni 4 zilizolipwa kwa wananchi kwaajili ya kupisha Mradi wa Makaa ya Mawe".alisema Bi. Tumaini
Tunakila sababu ya Kumshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi ya kuwahudumia wananchi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.