Na. Mwandishi wetu - Ludewa
Tarafa ya Mawengi Wilayani Ludewa imepata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Afisa wa Habari na Mawasiliano Serikalini Wilayani Ludewa Ndugu. Chrispin Kalinga amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi katika nyanja zote za Elimu, Afya, Maji, Barabara pamoja na Minara ya Mawasiliano ya simu.
Amesema katika nyanja ya Elimu kata zote zipatikanazo Tarafa ya Mawengi zimepata miradi kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwa ni pamoja na fedha za Mapato ya ndani na Fedha za Mradi wa Boost ambazo zimewezesha kujenga madarasa kwa baadhi ya kata ikiwemo kata ya Ludewa katika shule ya Msingi Ludewa Mjini ambayo imepokea fedha ya ujenzi wa madarasa 2 na matundu 6 ya vyoo ambayo tayari yamekamilika.
Aidha, akaongeza kwa kusema kuwa, kata zingine zimepata miradi ya ujenzi wa Hostel, pamoja fedha za ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Mawengi.
"Binafsi ninakila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutupatia fedha za kuteketeza Miradi hii mikubwa, lakini pia ninakila sababu ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga kwa kupaza sauti awapo bungeni na ndio maana leo miradi hii inaletwa kwenye Wilaya yetu" alisema Bw. Kalinga.
Akaongeza kwa kusema kuwa, akiwa Kama Afisa habari na Mawasiliano Serikalini ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa atahakikisha anaendelea kuipitia miradi yote na kuwahabarisha wananchi wote wa Wilaya ya Ludewa na watanzania wote kwa ujumla wake jinsi Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 invyotekelezwa kwenye kila kada ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Katika ziara yake iliyoanza Septemba 1 mwaka huu katika Tarafa ya Mawengi ametembelea miradi na kuhamasisha wananchi kufanya Utalii wa Ndani na kuvitangaza vivutio hivyo kwenye maeneo yao ambapo jana Septemba 03 amehitimisha ziara hiyo katika Tarafa ya Mawengi kwa kupanda Mlima Mrefu nyanda za juu kusini Mlima unaojulikana kwa jina la Livingstone - Madunda akiwa na zaida Vijana pamoja wananchi 120.
"Leo tumefanikiwa kuupanda Mlima Mrefu wa Livingstone wenye historia nzuri na ya kipekee, niwaombe wananchi wote wa Ludewa kuanza kufanya Utalii wa Ndani ya Wilaya yetu kwani hakuna mtu anayeweza kuutangaza Utalii kutoka nje Kama sio sisi wenyewe tutasimama na kuvitembelea, Serikali tayari tumeanza kuyafikia Maeneo yote ya vivutio vya Utalii na kuyafikia Maeneo hayo na ndio maana leo tupo hapa". Alisema Chrispin Kalinga
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.