Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imepanga kutoa mikopo kwa wavuvi wa Wilaya ya Ludewa kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo.
Akizungumza Mara baada ya kikao kazi na Vikundi binafsi vya Uvuvi, Vyama vya Ushirika vya Uvuvi lakini pia Makampuni ya Uvuvi Afisa Utumishi sekta ya Uvuvi Bi. Catherine Naaman amesema kuwa, serikali ipo tayari kuwakopesha boti na vifaa vyake vya Uvuvi kupitia Bank ya Kilimo (TADB ) kwa lengo la kuwaendeleza wavuvi wote wanaofanya shughuli hiyo ya uvuvi ndani ya Ziwa Nyasa kwa upande wa Wilaya ya Ludewa.
Sambamba na hayo amesema serikali inatoa mikopo isiyo na riba inayokwenda kuwasaidia wavuvi na wakuzaji viumbe maji, mradi huu utakwenda kusaidia kuongeza uzalishaji wa samaki utakaokwenda kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo.
Akaongeza kwakusema kuwa boti hizo zina urefu wa mita 7 hadi 14 zikiwa na injini zenye uwezo wa nguvu za farasi 9.9 hadi 60. Pia boti hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba wavuvi 6 – 20, kubeba Samaki tani 1.5, mtambo wa kufuatilia/kutambua uwepo wa Samaki (Fish finder), kifaa cha kuongoza boti (GPS), vifaa vya kuokolea Maisha na zana za uvuvi zikijumuisha mishipi na nyavu.
Kwa upande wake Afisa Uvuvi Wilaya ya Ludewa Prosper Kayombo amesema kuwa Moja ya malengo makubwa ya wavuvi wa Wilaya ya Ludewa ni kupata samaki wengi watakao kidhi mahitaji ya soko na changamoto kubwa iliyokuwepo ni pamoja na upatikanaji wa vifaa vya Uvuvi, Sasa serikali imewaona wavuvi wa Wilaya ya Ludewa na kuwakopesha fedha isiyo na riba kwalengo la kunyanyua vipato vyao na kuwapa vifaa vitakavyowasaidia katika kutekeleza mahitaji yao katika uvuvi.
Aidha akamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wavuvi wa Wilaya ya Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.