Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe Andrea Tsere leo tarehe 04/08/2022 amewapongeza wakulima wote wa Wilaya ya Ludewa waliopo kwenye maoneshe ya nanenane Jijini Mbeya kwa Upendo mkubwa waliouonesha kwa Wananchi wanaofika kutazama fursa mbalimbali kwenye banda la Wilaya ya Ludewa kwa kuwapa wananchi parachichi bure.
Kauli hiyo ameongea aliposhuhudia Wananchi wakishukuru wakalima hao mara baada ya kupatiwa elimu ya Kilimo bora cha parachichi na kupewa parachichi la kula.
Wananchi waliotembelea banda hilo wametoa hisia zao kwakusema kuwa, Maonesho ya nanenane ya Mwaka 2022 katika Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ni tofauti na miaka mingine kwa mpangilio mzuri wa mazao yao huku wakienda mbali zaidi kwakusema kuwa, Ludewa imeleta mazao na kutupatia elimu ya mazao yote lakini bado wakaona umuhimu wakutupatia na matunda bure hii ni kitu yakuigwa.
Mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Elvila amesema kuwa tumepata elimu ya Kilimo Cha bustani za mbogamboga nyumbani kwetu lakini pia wataalamu hawa wametupatia na mbegu za mbogamboga na kutushauli namna bora yakuzipika mboga hizo hivyo niwapongeze sana wataalamu kutoka Ludewa
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.