Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bwana Chrispin Kalinga amezungumza na Watanzania kupitia Redio Uplands Fm Njombe na kuwahamasisha kutembelea Banda la maonesho ya nanenane.
Katika mahojiano hayo Afisa Habari huyo alitumia nafasi hiyo kuwaeleza Watanzania kuwa Mkoa wa Njombe umejiandaa vyema kuwaonesha Watanzania fursa zilizopo Mkoa wa Njombe zikiwemo katika Kilimo cha Mahindi,Maharage,Kahawa,Korosho,Alizeti,Chai na Mazao mengine.
Sambamba na hayo alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha Watanzania kwenda Wilaya ya Ludewa kuwekeza katika sekta ya Kilimo lakini pia katika sekta ya Utalii.
Aidha Wilaya ya Ludewa imeshika nafasi ya pili Kitaifa kwa utoaji wa taarifa kwa Umma ikiwa ni pamoja na uhabarishaji wa taarifa za miradi mbalimbali pamoja mipango na mikakati inayotekelezwa kwenye Wilaya hiyo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.