Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana jana Februari 04,
2023 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Ludewa na kukagua
miradi mbalimbali inayotekelezwa na
Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) Wilayani Ludewa.
Pamoja na mambo mengine, amezindua zoezi la upandaji miti katika
wilaya ya Ludewa na kushiriki zoezi la upandaji miti zaidi ya 300
ambayo imepandwa katika eneo la shule ya sekondari Ludewa. Pia
ametembelea bweni linalojengwa katika shule ya sekondari Ludewa
Kwanza ambayo ni Shule Teule.
Aidha, Mhe. Waziri Balozi Pindi Chana amekabidhi gari moja lenye
thamani ya shilingi milioni 170 litakalotumika katika shughuli mbalimbali
za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilayani Ludewa.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliambatana na viongozi mbalimbali
akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Wise Mgina. Pia
walikuwepo Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga,
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa
wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndg. Stanley
Kolimba,Wakuu wa divisheni na vitengo wakiongozwa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert
Ngailo.
Wakati akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Ludewa katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mheshimiwa Waziri amepokea zawadi
ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan kutoka kwa umoja wa wanaweke wa Chama cha Mapinduzi
(UWT) Wilaya ya Ludewa. Zawadi hiyo imetolewa kama alama ya
shukrani kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna
anavyochapa kazi na kuipa Halmashauri ya Ludewa fedha kwa ajili ya
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.