Na. Chrispin Kalinga - Ludewa
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Barozi. Dkt. Pindi Hazara Chana leo tarehe 12 Oktoba 2023 amefanya kikao kikazi katika Ofisi ya Mkuu ya Wilaya ya Ludewa ambapo hapo amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva akiwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ezekiel Sandigila.
Kikao hicho kimehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias akiwakilishwa na Bw. Castor Kibasa, Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Walaya ya Ludewa, Watumishi wa Mahakama, Wakuu wa Divisheni na Wakuu wa Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa pamoja na Viongozi wa Taasisi za Umma.
Wakati akitoa salamu zake za serikali Mhe. Barozi Pindi Chana amesema kuwa kuwa, “Naomba nitumie nafasi hii kuwaasa wananchi wote wa Wilaya ya Ludewa na Watanzania wote kwa ujumla kutii sharia bila shuruti ili kudhibiti matukio ya kiuarifu, serikali imejipanga vyema kutokomeza matukio ya kiuvunjifu wa Amani na tupo tayar kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaovunja sharia, na kwasasa serikali inaendelea kuboresha na kuanzisha mahakama mbalimbali hapa nchini na tunajenga Magereza za kutosha.” Amesema Mhe. Pindi Chana.
Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania Mhe. Barozi. Dkt. Pindi Hazara Chana amemwagiza Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Ludewa kuhakikisha Gereza la Wilaya ya Ludewa linaingia kwenye Shirika la Maendeleo (SHIMA) Kwa lengo la kuwapatia ujuzi mbalimbali wafungwa wote wataoingia katika Gereza la Wilaya ya Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.