• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Ludewa District Council
Ludewa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uchumi
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
      • Maji
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Samaki
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Huduma za UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Kazi za Mwenyekiti Ofisini
  • Miradi
    • Miradi Iliyo Kwenye Mpango
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Habari Picha

WAZIRI WA HABARI NA MAWASILIANO ATOA SIKU 14 KWA MAAFISA HABARI NCHINI

tarehe Iliyowekwa: May 9th, 2022

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kuhuisha taarifa za Serikali kwenye tovuti za Serikali na mitando ya kijamii ili wananchi waweze kupata taarifa na kujua kinachoendelea kuhusu Serikali yao.


Akizungumza leo jijini Tanga wakati akifungua Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Waziri Nape amesema kuwa Maafisa Habari wa Serikali ni daraja linalorahisisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, hivyo ni muhimu kutimiza wajibu wao kwa kuwa na taarifa sahihi za Serikali na kwa wakati katika tovuti za Wizara au Taasisi zao.


“Natoa siku 14 kuanzia Mei 14 mwezi huu kila tovuti ya Serikali na mitandao ya kijamii iwe na taarifa za Serikali zinazoendana na wakati kuhusu utekelezaji wa Sera au miradi mbalimbali ya Serikali, Afisa atakayeshindwa kutekeleza hili tutaachana nae”, amesema Mheshimiwa Nape


Aidha, akiwa katika kikao hicho Waziri Nape ameiagiza Idara ya Habari – MAELEZO kuandaa mfumo utakaowezesha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano nchini kupatiwa mafunzo kuhusu miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini ili waweze kuwa na uelewa na kuweza kuisemea miradi hiyo, kuandaa mfumo wa Maafisa Habari kujadiliana masuala mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa pamoja na kuwa na mfumo wa kupima utendaji kazi wa Maafisa hao.


Katika hatua nyingine, Waziri Nape ameahidi kutatua changamoto ya uhaba wa Maafisa Habari katika ngazi ya Wizara na Halmashauri ili kuhakikisha Serikali ina wataalamu wa kuisemea katika ngazi zote.


“Nawaahidi hili liko ndani ya uwezo wangu la kusaidia kupata Maafisa habari katika mikoa ya Lindi, Manyara, Mbeya na Tabora na mikoa ya Dodoma, Kigoma na Geita mbayo Maafisa Habari wake wamekuwa Wasaidizi wa Wakuu wa Mikoa.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Kikao Kazi hicho kitandaa mkakati na kujifunza namna ambavyo dunia itahabarika kupitia Tanzania na kufikisha ujumbe wa maendeleo na namna ya watu kushiriki katika shughuli za maendeleo.


Pia Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa kuwa lengo la kikao kazi hicho cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini ni kujengeana uwezo wa namna bora ya kuisemea Serikali na kuwa atahakikisha maagizo yote yaliyotolewa yanatekelezwa ili kutimiza jukumu hilo kwa ufanisi.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI January 10, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III, NA WITO WA USAILI WA ANA KWA ANA KWA WALIOCHAGULIWA November 11, 2021
  • TAADHARI YA UGONJWA WA POLIO LUDEWA March 24, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA KATIBU MAHSUSI III NA DEREVA II May 25, 2022
  • Tazama zote

Habari za Punde

  • MKUU WA WILAYA LUDEWA AUNGANA NA WANANCHI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUSAFISHA MAZINGIRA

    June 05, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA WILAYANI LUDEWA NA KUTEMBELEA MIRADI MITANO(5)

    May 07, 2025
  • WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. SELEMANI JAFO AAHIDI KUANZISHWA KWA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA HIVI KARIBUNI

    February 19, 2025
  • ZIARA YA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, MHE. DKT. SELEMANI JAFO MKOANI NJOMBE, WILAYANI LUDEWA.

    February 17, 2025
  • Tazama zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Dira na Dhima
  • Utawala na Rasilimali Watu
  • Historia
  • Misingi Mikuu
  • Orodha ya Madiwani
  • Miradi Iliyokamilika

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais IKULU
  • Tovuti Kuu ya Wananchi
  • Wizara ya Afya
  • Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  • TANePS

Wanaotembelea Tovuti

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ludewa - Njombe

    Sanduku la Barua: 19

    Simu: 026-2790120

    Simu ya Rununu:

    Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.