Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, (Mb) ameipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Kuratibu vyema mashindano mbalimbali yanayofanyika ndani na nje ya nchi ambayo yameendelea kuitangaza vyema Tanzania.
Pia ametoa rai kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI zihakikishe kuwa Sekta ya michezo inaendelea kupewa kipaumbele katika ngazi zote hapa nchini.
Mhe. Kassim Majaliwa ametoa pongezi na rai hiyo leo Aprili 13, 2023 Bungeni jijini Dodoma alipokutana na Mabingwa wa Soka Afrika kwa upande wa Shule za Sekondari, timu ya Fountain Gate waliofika Bungeni jijini Dodoma kupongezwa kwa kutwaa Ubingwa huo.
"Naupongeza Uongozi wa Shule hii pamoja na Alliance ya jijini Mwanza kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuunga mkono maendeleo ya Sekta ya Michezo nchini, tunawashukuru sana naamini mtaendelea kufanya hivyo katika michezo mingine" Amesisitiza Mhe. Majaliwa.
Ametumia nafasi hiyo kuipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuendelea kufanya vizuri katika maendeleo ya Sekta zake, ambapo pia amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa kufanya mabadiliko katika Shirikisho hilo ambalo sasa mafanikio ya mchezo wa Soka yanaonekana.
Aidha, ameagiza Wizara ya Elimu, TAMISEMI na Wizara ya Utamaduni kuhakikisha somo la michezo linafundishwa shuleni kwa kuwa waalimu wa somo hilo wapo katika chuo cha Malya na Butimba.
Mhe. Majaliwa ameagiza pia mchezo wa Netiboli upewe kipaumbele na uanze kufanyika kwakua ni miongoni mwa mchezo uliokua unafanya vizuri ndani na nje ya nchi.
Awali, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara itaendelea kuratibu mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa kuwa ni miongoni mwa mashindano yanayozalisha wachezaji wengi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.