WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amefungua kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano serikalini huku akibainisha mafanikio yaliyopatikana katika miaka miwili ya uongozi wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ikiwamo utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi.
Programu hiyo inatekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, ambapo katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Februari, 2023 vijana 37,193 wamenufaika kwa njia ya uanagenzi, mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana katika mfumo rasmi, mafunzo kwa Utarajali, mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba na mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio kazini.
Akifungua kikao hicho leo Machi 27, 2023 jjini Dar es salaam ulioratibiwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na ldara ya Habari Maelezo, Mhe.Majaliwa amesema mafanikio hayo ya programu hiyo yamefahamika kwa wananchi utokana na kuchagizwa na ushiriki wa tasnia ya habari.
"Hivi karibuni Machi 20, 2023 tumeshuhudia Mheshimiwa Rais akizinduaprogramu ya kwanza ya mafunzo kwa vijana wapatao 800 ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Building Better Tomorrow (BBT) kwa kuwapatia vijana maeneo ya kulima kwenye vitalu'alimesema.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.