Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambaye pia ni Mbunge wa Mkoa wa Njombe (Viti Maalum), alikabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na mabati 152 katika Shule ya Sekondari Madilu iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Mhe. Chana alikabidhi vifaa hivyo Julai 1, 2023 shuleni hapo ambapo aliwasitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii, kuongeza nidhamu pamoja na kuonesha vipaji vyao katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa ni miongoni mwa sekta zenye fursa ya ajira kwa sasa.
"Masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo lazima yapewe kipaumbele, kila shule inayosajiliwa lazima kuwe na miundombinu ya michezo ambapo katika shule 56 za michezo zilizotengwa zikiwemo Matola na Makambako za Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa shule zitakazokarabatiwa kwa ajili ya kukuza michezo, amesema Mhe. Chana
Aliongeza kuwa, katika mwaka huu wa fedha wizara itatekeleza Programu ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mtaa kwa Mtaa ambapo amesisitiza jamii kutobadilisha matumizi maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo pamoja na kuyalinda.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Victoria Mwanziva aliwataka wazazi kusimamia wanafunzi wa shule hiyo na nyingine kuhudhuria masomo, pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo katika wilaya ya Ludewa.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), badhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mhe. Wise Mgina walihudhulia tukio hilo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.