Mkuu wa Wilaya ya Ludewa asherehekea Siku ya Wazee Duniani na Wazee wa Wilaya ya Ludewa.
Kila tarehe Mosi Oktoba kila mwaka huwa ni Maadhimisho ya siku wa Wazee Duniani ambapo wazee hukumbukwa kwa michango yao mbalimbali hasa kwa kuyatumikia mataifa yao katika Nyanja mbalimbali wakati wa ujana wao.
Wilaya ya Ludewa ni Miongoni mwa Wilaya zilizoshiriki siku hii hapa nchini Tanzania kwa kuwakusanya Wazee kutoka kwenye maeneo mbalimbali ili kusheherekea siku hii ya Wazee Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa akiwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Bwn. Linus Malamba wakati akiongea na wazee wa Wilaya ya Ludewa amewaasa vijana kuiga ubunifu kutoka kwa wazee hao ambao walilitumikia Taifa la Tanzania kwa moyo mmoja na kuazisha viwanda mbalimbali nchini ili kuinua uchumi wa nchi.
Wazee hawa walianzisha mashamba ya kahawa,chai pia na kuanziasha viwanda vya aina mbalimbali nchini na kuviendesha lakini vijana wa siku hizi hawafanyi kazi bali wanakaa vijiweni na kucheza mchezo wa pool . Nawaasa vijana mkakae na wazee na muwaulize mbinu walizokuwa wanazitumia katika kufanya kazi mbalimbali na kuendesha familia.
Wazee wameishukuru Serikali kwa kuwakumbuka katika siku hiyo na kuwapa huduma za mara kwa mara. “Kwanza sisi wazee tuliopo hapa tulikuwa hatujui kama leo ni siku yetu Duniani lakini kwa kuwa Mkuu wa wetu wa Wilaya ametukumbuka nasi tumefurahi sana tumeona tunavyothaminiwa. Alishukuru Mwenyekiti wa Wazee.
Aidha, Mzee aliongeza kwa kusema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwapatia vitambulisho vinavyowatambulisha Pindi wanapohitaji huduma ya matibabu ya kutibiwa ambapo hapo awali walikuwa wakipata tabu ya kwenda kutibiwa Hospitali kwasababu ya kukosa fedha za matibabu.
Katika Maadhimisho hayo wazee hao wameiomba serikali kuwasaidia na wao Kama wazee kupatiwa mikopo isiyo na riba kwani bado uwezo wa kufanya kazi wanao na wanamatumaini yakuendeleza nchi kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijasiliamari.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa akiwakilishwa na Bwn. Girbet Ngailo amewasihi wazee hao kuwahamasisha vijana kufanya kazi za kuwaingizia kipato na kuacha tabia ya kucheza puru muda wote.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.