Na. Chrispin Kalinga - Ludewa
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ni miongoni mwa Halmashauri nchini Tanzania zilizoshiriki maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani kwa Mwaka 2023 ambapo kila Mwaka siku hii hufanyika ifikapo tarehe 01 Oktoba.
Jana tarehe 02 Oktoba 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa iliwakusanya zaidi ya Wazee 80 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ludewa na kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujengewa uelewa na hamasa kuhusu kulinda haki, Ustawi na Maslahi ya Wazee.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias ndiye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo kiwilaya yalifanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa katika siku hiyo ilikuwa ni pamoja na mijadala ya Wazee, kudhibiti mmong'onyoko wa maadili, Ukatili na fulsa Kwa Wazee. Lakini pia zilitolewa huduma mbalimbali kwa Wazee ikiwa ni pamoja na huduma za afya za Upimaji wa Blood presure na Macho Bure.
Afisa Lishe wa Wilaya ya Ludewa alipata nafasi ya kutoa elimu kwa Wazee inayohusiana na Lishe bora kwa Wazee lakini pia kwa Watoto wanaoishi nao.
Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani kwa Mwaka 2023 yameongozwa kwa kauli mbiu isemayo *"Uthabiti wa Wazee kwenye Dunia yenye Mabadiliko.*
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.