Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani huadhimishwa katika nchi nyingi duniani kila mwaka mwezi Machi 8.
Ni siku ambayo wanawake wanatambulika kwa mafanikio yao bila kuzingatia migawanyiko, iwe ya kitaifa, kikabila, kiisimu, kitamaduni, kiuchumi au kisiasa.
Tangu miaka hiyo ya awali, Siku ya Kimataifa ya Wanawake imechukua mwelekeo mpya wa kimataifa kwa wanawake katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Wanawake wa Wilaya ya Ludewa kuelekea wiki la kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake wamefanikiwa kushiri shughuli mbalimbali Wilayani Ludewa na kutenda matendo ya huruma katika kata ya Mundindi ambapo tarehe 7 walifanikiwa kutembelea shule ya watu wenyemahitaji Maalumu iliyopo kata ya Mundindi Wilayani Ludewa.
Aidha walifanikiwa kutoa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja Daftari, Sabuni Mavazi nk.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Castori Kibasa akiwakilishwa na Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Ahobokile Songera alishiriki maadhimisho hayo kiwilaya.
Wanawake wa Wilaya ya Ludewa leo Machi 8, 2023 wameshiriki maadhimisho hayo kimkoa ambapo Machi 11, 2023 Wanawake wa Wilaya ya Ludewa wanatarajia kufanya tathimini ya ushiriki wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake katika Ukumbi wa Sehemu kubwa na kuifanya siku hiyo kuwa ni ya kipekee kwa kusheherekea na kuipa siku hiyo jila la "Usiku wa Mwanamke
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.