Jana Oktoba 09, 2022 Wananchi wa Kijiji Cha Ludewa Mjini wameshiriki mkutano wa kijiji huku ikiwa ni pamoja na kusomewa mapato na Matumizi ya Kijiji hicho.
Wakati akisoma mapato na Matumizi ya Kijiji hicho mhasibu wa Kijiji hicho Bi. Yustar Ngalawa alisema kuwa, Viongozi wote wa kijiji wanafanya kazi yakuwatumikia wananchi na kuhakikisha Matumizi na ukusanyaji wa mapato unafanywa kwa weredi wa hali ya juu.
Wananchi waliohudhulia mkutano huo walilidhiwa na kumpa zawadi mhasibu huyo kwa kutunza na kutoa taarifa sahihi na zenye uhakika.
Aidha mkutano huo ulijadili mambo mbalimbali ikiwa nipamoja na ushiriki wa maendeleo ya Wananchi haswa wakati huu wa jua Kali haswa kwenye uandaaji wa tofari za kutekeleza Miradi mbalimbali.
Katika hatua nyingine mkutano huo uliambatana na utoaji elimu ya Uraia ambapo A/INSP Naftari Mwinuka alitoa elimu ya Uraia na kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli za Maendeleo kwani Wilaya ya Ludewa hujengwa kwa kushiriki Shughuli za maendeleo.
Sambamba na hayo Afisa Mifugo wa Kata hiyo alitumia nafasi ile kuwakumbusha wananchi wote wa kata ya Ludewa kuilea mifugo yote kwa wakiwemo Nguruwe na Mbwa na kuhakikisha mbwa wote wanapata Chanjo ya kichaa cha mbwa
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.