Na. Chrispin Kalinga - Ludewa
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi kwa makundi mbalimbali ya kijamii na wanafunzi wa Wilaya ya Ludewa ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea kutokana na utumiaji wa dawa kiholela.
zoezi hilo limefanyoka leo Oktoba 17, 2023 katika shule ya Sekondari St. Alois iliyopo Wilayani Ludewa na wananchi waliofika kupata huduma za kiafya katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo mkaguzi wa dawa BW. Adam Sarota amesema mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu pamoja na kujifunza kutoa taarifa ya madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa hizo.
Aidha, amesema matumizi yasiyo sahihi ya dawa na vifaa tiba na vitendanishi yanasababisha athari kubwa kwa watumiaji, watu kupoteza maisha, kupata ulemavu na viungo mbalimbali kuathirika kama ini na, figo.
Sarota alisema utoaji wa elimu hiyo itakuwa endelevu ili wananchi waweze kujua namna bora ya matumizi ya dawa na ndio maana wameanzisha klabu za TMDA katika shule za mkoa wa Njombe mbalimbali ili elimu hiyo inayotolewa na TMDA iweze kusambaa kila maeneo na kuifanya jamii kuelewa athari za matumizi ya dawa hizo.
Mkaguzi alitoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya dawa ikiwemo kuepuka matumizi holela ya dawa kwa kutumia dozi kikamilifu sambamba na kupata vipimo na ushauri wa wataalam wa Afya kabla ya kutumia dawa hizo.
"Kuna baadhi ya watu katika jamii wanatumia dawa kiholela na sisi TMDA tunaendelea kuwaelimisha kuwa utumiaji wa dawa kiholela unaweza kusababisha usugu wa vimelea na kufanya dawa hizo kushindwa kufanyakazi kama inavyotakiwa" alisema Sarota
Aidha aliwataka wanafunzi hao kufikisha elimu hiyo kwa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla kwa lengo la kuendelea kulinda afya ya jamii
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.