Na Chrispin Kalinga - Ludewa
Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watumishi kutoka Halmashauri Wilaya ya Ludewa, jana tarehe 10 Mei, 2023 walifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Ludewa, lengo likiwa ni kuimarisha utendaji kazi na kuhamasisha ukimbizwaji wa utekelezaji wa Miradi hiyo.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa walipata fursa ya kutembelea Jengo jipya lililokamilika pamoja na kutazama vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa kwaajili ya wagonjwa mahututi vya jengo la ICU.
Aidha, ziara hiyo ilianza kwa kikao kilichofanyika katikaUkumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya wilaya ya Ludewa ambapo kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mhe. Wise Mgina, ambapo walipata nafasi yakujadiliana mambo mbalimbali sambamba na Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi na Mipango pamoja na timu ya Menejimenti Halamashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa Wataalm wa Halamashauri ya Wilaya ya Ludewa, waliwaeleza waheshimiwa Madiwani kuwa wao kama wataalaam wamejinga kisawasawa kuibua vyanzo mbalimbali vya mapato na kuwa kinara mara kwa mara katika ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuelekea Msimu huu mpya wa kiangazi ambapo mvua zimepungua na kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na waheshimiwa Madiwani ni pamoja na Jengo Jipya la Utawala, Jengo jipya la nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Ukaguzi wa Majengo mbalimbali yanayojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ludewa pamoja na ukaguzi wa jingo jipya linalojengwa katika shule ya Vipaji ya sekondari ya Ludewa Kwanza (Ujenzi wa Hostel).
"Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ina miradi mikubwa kulingana na uwekezaji unaotokana na Mapato kuwa mazuri, pia uwepo wa miradi ya kimkakati Kama Standi ya Mabasi inayoyojengwa katika Kata ya Madope pamoja na Miradi mingine inahitaji kutekelezwa kwa wakati ili kuondokana na mlundikano wa miradi kuwa mingi na kushindwa kuliza kwa wakati, naomba nitumie nafasi hii kuwaelekeza mafundi wote mlioshika majengo yetu mtekeleze kwa wakati kama mikataba ya makubaliano ya utekelezaji tulivyokubaliana” alisema Mhe. Wise Mgana.
Ziara hiyo ilifanyika kuelekea Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani unaotarajia kufanyika tarehe 13 Mei 2023 katika Ukumbi wa Halmashauri kuanzia saa mbili kamili asubuhi, Wananchi wotw mnakaribishwa kushiriki Mkutano huo.
--
God is the first in the world
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.