Wananchi wa Wilaya ya Ludewa wanaendelea kuuza mahindi katika maghala yaliyo tengwa ikiwa ni pamoja na ghala la Shaurimoyo wilayani hapo.
Shirika la hifadhi ya chakula NFRA linaendelea kununua mahindi kwa wananchi kwenye vituo vyote vilivyotengwa kwani huwarahisishia wakulima kwa kuwafuata hukohuko ukilinganisha na miaka mingine.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ludewa Bi. Clementina Kabaka amewapongeza wakulima wote wanaoendelea kusogeza mahindi yao katika maghala hayo na kuwasihi wakulima kutumia wakala wa chakula NFRA kuuza mahindi yao kwani bei zao ni nzuri ukilinganisha na miaka mingine ambapo kwasasa bei ya mahindi kwa kilo moja ni shilingi 800.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.