Mtendaji wa kata ya Lifuma amepata wasaa wa kuwahimiza wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi mwaka 2023 katika shule ya Msingi Lifuma na kuwaambia kuwa wanapaswa kufanya mitihani yao vizuri ili wapate ufaulu unaoheshimisha Kata yake na akaongeza kwa kusema kuwa kumekuwa na Wazazi na Walezi wanaowaelekeza watoto kujifelisha mtihani kwamadai hawana uwezo wa kuwasomesha, sasa Serikali ya awamu ya sita imefuta ada kuanzia shule ya Msingi hadi kidato cha sita.
Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akitembelea miradi inayotekelezwa kwenye kata hiyo alipokuwa na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wakati wa Ziara yake ya Tarafa ya Mwambao
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.