Na Mwandishi wetu
Tarafa ya Mwambao Wilayani Ludewa ya neemeka kwa miradi mbalimbali ya maendleo inayotekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akielezea miradi hiyo Afisa wa Habari na mawasiliano serikalini Wilayani Ludewa Ndg. Chrispin Kalinga amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi katika nyanja zote za Elimu, afya, usafiri wa majini ja miundombinu ya barabara.
Amesema katika nyanja ya Elimu kata zote zipatikanazo Tarafa ya mwambao zimepata miradi ya kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwa miongoni ni TASAF na Fedha za Boost ambazo zimewezesha kujenga madarasa kwa baadhi ya kata wengine wakipata miradi ya nyumba za walimu na ofisi yote hii ni kuhakikisha huduma ya elimu inakuwa bora ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Ameongeza kuwa serikali imeongeza idadi ya watumishi katika maeneo mbalimbali ndani ya Tarafa ya Mwambao na Wilaya nzima ya Ludewa ikiwa na adhima ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati na za uhakika katika maeneo yao
Akiongelea miundombinu ya barabara Kalinga amesema shughuli za ufunguzi wa barabara ziendazo mwambao zina endelea na lengo ni kuhakikisha Tarafa ya Mwambao inafikika kwa gari kwani awali kulikuwa hakuna barabara za kuwafikisha huko.
Kwa upande wa mawasiliano ya simu amesema Serikali imeendelea kupeleka huduma ya mawasiliano katika maeneo yote ya mwambao na kupelekea kupunguza changamoto waliyo kuwa wakipitia awali ya kusubiri mpaka jua liwake ndio wapate huduma kwani sasa imejengwa minara ambayo inatumia nishati ya mafuta na sio jua tena.
Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga kwa kuendelea kuipigania na kuisemea Wilaya ya Ludewa kwani jitihada zake zinaonekana na zinazaa matunda Wilayani humo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.