Na. Chrispin Kalinga
Mgeni Rasmi katika siku ya pili ya Tamasha la Pili la Utamaduni Kitaifa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Agosti 26, 2023 amekagua mabanda ya maonesho ya Utamaduni na Sanaa pamoja na huduma mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali, Fedha na Wadau wengine.
Mhe. Chana ameongozana na viongozi mbalimbali kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko, viongozi wa mkoa wa Njombe wakiongozwa na muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, Wakuu wa Idara za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mheshimiwa Victoria Mwanziva ameshiriki Tamasha hilo huku viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa akiwemo Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Ludewa, Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa pamoja na wananchi wa Wilaya ya Ludewa wameshiriki.
Tamasha hilo la Kitaifa linalofanyika mkoani Njombe linaongozwa na kaulimbiu inayosema Utamaduni ni Msingi wa Maadili, tuulinde na kuuendeleza.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.