Januari 31, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ngailo walipo watembelea wananachi wa kijiji cha Maholong’wa waliofikwa na maafa yaliyosababishwa na Mvua iliyo nyeshaJanuari 27, 2023.
Mvua hiyo iliyo ambatana na upepo mkali ilipelekea kuezuliwa kwa jengo moja la Shule ya Msingi Maholong’wa, nyumba 28 za wananchi, ekari 135 za Mahindi na ekari 23 za maharage.
Akizungumza na waathirika wa maafa hayo Mhe. Mkuu wa Wilaya alimwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Ludewa kukarabati darasa la shule ya msingi Maholong’wa lililo ezuliwa na mvua ili wanafunzi wa darasa hilo waweze kutumia upya darasa lao.
Aidha aliipongeza kikosi kazi kilichoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwaajili ya ujenzi na kukarabati nyumba zilizohalibiwa na mvua na kuwaomba waongeze juhudi ili wahanga warudi kwenye makazi yao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ngailo aliwajuza wananchi waliokumbwa na maafa hayo kwakusema kuwa, Serikari imetambua madhara yaliyojitokeza na kuona umuhimu wa kuleta mbegu za mazao za kisasa Zaidi ya tani 1 ambazo zitauzwa kwa wananchi kwa bei pungufu na mbegu hizo zinastawi ndani ya mda mfupi (siku 60 - 65).
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.