Leo Mei 10, 2022 Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akiongozana na Maafifa Habari na Uhusiano wa Serikali wametembelea Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga kwa lengo la kujionea maendeleo ya upanuzi huo.
Serikali imetoa jumla ya bil. 256.8 kwa ajili ya kuboresha bandari ya Tanga kwa awamu ya pili ili kufanya upanuzi wa bandari kwa kujenga gati mbili zenye upana wa mita 150 na urefu wa mita 450 kupunguza adha ya ushushaji wa mizigo baharini na kugharimu mamilioni ya fedha.
Taarifa hiyo imetolewa na Mhandisi wa bandari ya Tanga Mhandisi Hamis Omary Kipelo wakati akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika ziara ya maafisa habari,Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali iliyofanyika leo katika bandari hiyo ili kutembelea mradi wa ujenzi wa mageti ya kushushia mizigo yanayojengwa na kampuni ya China Urban
Mhandisi Kipalo amesema kuwa maboresho ya bandari ya Tanga yamefanyika kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza kazi zilizofanyika ni kuongeza kina kwenye lango la bahari na kuchimba eneo la kuingilia bahari na kugharimu jumla ya shilingi Mil. 172.8 ili kupunguza umbali wa kufuata mizigo baharini kutokana na kukosekana kwa geti za kushushia mizigo katika bandari hiyo.
Amesema kuwa zamani meli ilipowasili mzigo ulifuatwa kwa umbali wa kilomita 1.7 kutoka bandarini lakini baada ya Serikali kuamua kuongeza kina cha kuingia kwenye lango la bahari umbali kufuata mizigo umepungua na kufika mita 200 kutoka bandarini na gharama za uendeshaji wa operesheni zimepungua.
Naye Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu Wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa endapo mradi huo ukikamilika utapunguza gharama za kushusha mizigo na wananchi watanufaika kupitia bandari hiyo na kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es salaam kwani nchi jirani kama Rwanda,Burundi,Uganda na Kongo zinaweza kutumia bandari ya Tanga.
Bandari ya Dar es salam jumla ya trilioni moja inatumika kupanua njia ya kupita meli kubwa lakini pia bandari mbalimbali ikiwemo bandari ya Kalembo imefikia 98,bandari ya mtwara maboresho yamefanyika na sasa imekamilika na inauwezo wa kuhudumia tani milioni moja kwa mwaka,na serikali inafanya jitihada ya kuunganisha kutoka Mtwara,Mbamba bay na kuhudumia Nchi ya Malawi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.