Mtendaji wa Kata ya Lugarawa Bw. William Devid Kachoko ametuma salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha kata ya Lugarawa zaidi ya Bilioni 7.5 za kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na iliyokamilika utekelezwaji wake.
Ametuma salamu hizo katika ziara ya kikazi ya Afisa Habari na Mawasiliano serikalini ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa akitembelea miradi inayotekelezwa kwenye Tarafa ya Liganga na Tarafa ya Mlangali
Mtendaji huyo amemshukuru Diwani wa kata hiyo kwakuendelea kuwa mnyororo mzuri na kuyawakilisha vyema maombi ya wananchi wa kata hiyo kwa Mheshimiwa mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga na sasa utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 inatekelezwa kwa kishindo katika kata ya Lugarawa ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa rami katika barabara za mitaa, ujenzi wa chuo kikubwa cha Ufundi VETA, uboreshwaji wa miundombinu ya umeme na miradi mingine ya Elimi, Afya na Maji.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.