Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Mawakili wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uaminifu.
Amewataka Mawakili wote wa Serikali wakati wa kutekeleza
majukumu yao watambue kuwa wamekabidhiwa dhamana
kubwa ya sekta ya haki.
Ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa chama cha Mawakili wa Serikali ambapo pia amezindua chama cha Mawakili hao wa Serikali.
Amesema ni muhimu kwa Mawakili wa Serikali kutambua kazi ya kusimamia haki iko mikononi mwao na kwamba wananchi wengi wanahitaji msaada wa kisheria kutoka kwao.
Rais Samia amesema katika uongozi wake anatamani kuona
Mawakili hao wa Serikali wanatenda haki wakati wa kuhudumia wananchi na wawasikilize pamoja na kutatua shida zao.
Kwa upande wa Serikali, Rais Samia amesema itaendelea
kutenga fedha kwa ajili ya sekta ya sheria wakiwemo Mawakili
wa Serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Pia amewapongeza kwa kuanzisha mfumo wa Mawakili wa Serikali na kuwataka Mawakili ambao hawajajisajili katika mfumo huo kufanya hivyo mara moja.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.