Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na wananchi wa Makete leo Agosi 9,2022 ambapo amefungua barabara ya Njombe-Makete (107 km) na kuahidi kutoa Milioni 100 kwa ajili ya kuweka taa za barabarani Makete mjini
Pia amewaagiza Viongozi ngazi ya Wilaya kwa kushirikiana na wananchi kuchanga fedha kiaisi cha shilingi Milioni 100 ili kuongeza Taa za barabarani na kufikia Kilomita 2 na kuunga mkono jitihada za Serikali katika uwekaji wa taa hizo.
Mhe. Rais amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Njombe-Makete hivyo amewataka wananchi kulinda na kutunza miundombinu ya Barabara hiyo.
Pia amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Lami kutoka Makete-Mbeya ambapo kwa kuanza Serikali inaanza mwezi wa tisa (9) mwaka huu kujenga Kilomita 36 kutoka Iniho kuelekea Kitulo eneo ambalo ni korofi sana na fedha zitaendelea kutengwa ili kukamilisha barabara hiyo yenye umuhimu mkubwa kiuchumi kwa wananchi wa wanamakete.
“Mkandarasi amepatikana tayari na ujenzi unaanza mwezi wat isa barabara hii ni muhimu kwa kukuza utalii katika Wilaya ya Makete, kuongeza shughuli za uzalishaji na niwapongeze kwa upandaji wa miti kwa wingi katika Wilaya hii, niwasihi kabla hatujakata miti tuhakikishe tumepanda mingine mingi ili kutunza mazingira yetu”.
Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga akizungumza mbele ya Rais na wanamakete sambamba na kumshukuru Mhe. Samia kwa ujenzi wa Barabar, Shule ya wavulana Makete, kutoa fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na Jengo la Halmashauri, ujenzi wa Bwala la Umeme Lumakalya na miradi mbalimbali ameongeza kuwa changamoto kubwa ambayo inabeba hitaji la wanamakete kwa sana ni barabara ya Lami kutoka Makete-Mbeya.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.