Mfumo wa Kuimarisha Sekta ya Umma (PS3) ni mradi wa miaka mitano unaofadhiliwa na Watu wa Marekani (USAID) nchini Tanzania. Lengo la PS3 ni kuimarisha mifumo ya serikali katika ngazi zote za kitaifa na za mitaa ili kuboresha upatikanaji, matumizi na ubora wa utoaji wa huduma katika sekta za afya, elimu na kilimo, kwa kuzingatia watu wasikuwa na uwezo (undersaved). PS3 inafanya kazi chini ya vipengele vitano: uongozi na ushiriki wa wananchi, rasilimali za binadamu, usimamizi wa kifedha, mifumo ya habari na utafiti wa shughuli.
Mradi unatarajia kuendesha mafunzo kwa muda wa siku mbili kwa Wahehimiwa Madiwani wote katika Halmashauri za mkoa wa Njombe kuanzia tarehe 4 mpaka 5 mwezi wa 4, 2017. Waalikwa ni wafuatao;
1. Waheshimiwa Madiwani wote
2. Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote
3. Maafisa Utumishi wa Wilaya zote
4. Karani wa Baraza la Madiwani
5.Mratibu wa Mradi ngazi ya Wilaya
Pia Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya zote na Makatibu Tawala wa Wilaya wanaalikwa katika Mafunzo haya.
Muda wa mafunzo ni kuanzia saa 1.30asubuhi kila sikuy, hivyo washiriki watapaswa kufika Njombe siku moja kabla.
Kwa Mawasilianao zaidi piga simu kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya au wasiliana na Mratibu wa PS3 Wilaya
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.