Muhunzi wa zana mbalimbali kutoka Mkoa wa Njombe aitwaye Reuben Mtitu maarufu kama Mzee Kisangani kutoka wilayani Ludewa leo Januari 07, 2023 ametembelea Banda la wizara ya Madini na kubadilishana uzoefu wa namna ya kubadili makaa ya Mawe kuanza kutumika kwa Matumizi ya nyumbani.
Mhunzi huyo ambaye wengi sasa wamezoea kumuita Prof. Kisangani alibuni mitambo mbalimbali ya kutengeneza vyuma, na nyenzo mbalimbali na hivi sasa ameanzisha chanzo cha umeme wa maji kinachohudumia wananchi zaidi ya 25 wilayani Ludewa.
Leo ametoa mawazo yake ambapo licha ya kusema kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kuanza kuchakata mkaa utakaotokana na Makaa ya Mawe yanayopatikana wilayani Ludewa.
Kisangani amesema kuwa ujio wake Zanzibar ni kuangalia soko la bidhaa anazotarajia kuanza kuzalisha lakini pia usambazaji wa Parachichi anazolima kutoka Ludewa.
Mwisho akamaliza kwa kusema kuwa, Nane nane ya Mwaka huu Jijini Mbeya anatarajia kupeleka Majiko yatokanayo na Madini ya Chuma lakini pia kupeleka mkaa utakaotumika majumbani utokanao na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma toka Ludewa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.