Amka asubuhi na mapema jua likichomoza upate kuona jua likichomoza na maadhari ya ajabu ya safu za Milima ya Livingstone inayoishia kwenye Ziwa Nyasa.
Ziwa Nyasa limezunguka Ukanda wa Mbeya Ludewa bila kusahau Ruvuma, huko kote kuna vitu mbalimbali vinavyo wafanya watu wengi kutamani kuishi na kuendelea kuyafurahia mazingira na safu za Milima iliyo pendezesha Ziwa Nyasa,
Pamoja na mambo yote huduma muhimu kama vile Hoteli, na Vyakula havijakosekana na unapo fika kutalii ndani ya Ziwa Nyasa utakula vyakula asili kama vile Ugali wa Muhogo,Samaki wa Ziwa Nyasa, Dagaa nk
Usiku kucha utafurahia kuwapo maeneo yote yaliyo zungukwa na Ziwa Nyasa kama vile Manda, Lupingu, Makonde, Matema bila kusahau Ruvuma na kwenginepo.
Ili asubuhi na mapema uweze kufurahia Jua kutoka Upande wa juu itakulazimu ukeshe huko na ushuhudie Mwangavu mzuri wenye kukufanya ujione upo paradiso nasi Wana Ludewa pamoja na Watanzania wote tunajivunia Ziwa Nyasa na tunakubali kuwa Wilaya ya Ludewa ni moja ya Wilaya zilizo barikiwa na Mungu kwa upekee wa utajiri uliopo humo.
Mambo ya kufanya ukiwa Ziwa Nyasa,Kutembelea na kujionea Samaki wenye rangi nzuri zenye jina la Samaki wa Mapambo,Kutembelea Milima iliyo pangwa na Mungu kwa mtiririko unao someka kwa ZZZ,lakini pia kushuhudia Mawimbi ya aina yake mazuri yanye kukufanya utamani kuhamia huko na kwa mbaaali unapaswa kusikia sauti za ngoma za asili zilizo changamana na Firimbi huku ukitafuna ytaratibu dagaa Nyasa wenye utamu ulio tukuka.
Majira ya asubuhi Shughuli mbalimbali zinaendelea ikiwemo Uvuvi, Kuogelea, Kustarehe na Kutembelea Mapango na mito pamoja na mengineyo mengi yaliyopo huko.
Jinsi ya Kufika huko
Unaweza kuendesha gari kutoka Njombe hadi Manda na Kutoka Ludewa hadi Lupingu na huko utapata Meli, Boti na Mitumbwi ya kukufikisha popote unapo hitaji.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.