Na Chrispin B. Kalinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema nyongeza ya mshahara ya kila mwaka kwa Watumishi wa Umma ambayo ilikua imesimama kwa muda mrefu itaanza kuzingatiwa mwaka wa fedha 2023/ 24 na kuendelea kwa miaka ijayo.
Mhe. Samia amesema hayo Mei Mosi 2023, mkoani Morogoro wakati akihutubia katika siku ya wafanyakazi iliyoadhimishwa Kitaifa mkaoni Morogoro.
“Nawahakikishia kuwa, katika uongozi wangu Madaraja yataendelea kupanda, mafao ya wastaafu yatalipwa kwa wakati, kubadilisha kada itazingatiwa na waliondolewa kazini wataendelea kulipwa stahiki zao”, alisisitiza Mhe. Samia.
Akaongeza kwa kusema kuwa, Serikali inaendelea kulipa madai ya wafanyakazi baada ya kumaliza uchambuzi wa madai hayo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mawaziri akiwemo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na viongozi wengine wa Umma na Binafsi pamoja na wanachi wa Mkoa wa Morogoro.
Aidha, sherehe hizo zilimepambwa na Maandamo ya wafanyakazi wakiwa na ujumbe mbalimbali wakiwemo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni Mishahara Bora na Ajira zenye Staha ni nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.