Hizi ni nukuu mbalimbali zinazotuvusha juma la pili la mwezi Februari 2023 endelea kutembelea mitandao yetu ya Kijamii kujipatia habari na taarifa mbalimbali kutoka ndani ya Wilaya ya Ludewa.
"Miti hii tunayoitoa kwa wananchi tunalengo la kuhakikisha kila eneo la Wilaya ya Ludewa lenye sifa ya kupandwa miti linaoteshwa kwa lengo la kutunza mazingira na kumwingizia kipato mwananchi"
##RamadhanSaid
#MhifadhiMisitu (W) Ludewa.
"Kwa mwaka 2022/2023 zaidi ya miche ya miti 30,000 tumezipatia taasisi za serikali na binafsi. Taasisi hizo tayari zimeipanda miti hiyo na zaidi ya miti 20,000 tumevipatia vikundi na miti 10,000 tuwewapatia watu binafsi na yote tayari imepandwa"
#RamadhanSaid
#MhifadhiMisitu (W) Ludewa.
"Uchomaji Moto kwa Wilaya ya Ludewa ulikithiri kwa mwaka 2021/2022 kutokana na kuwepo kwa kipindi kirefu cha jua kali. Ila kwa mwaka 2022/2023 uchomaji Moto ulipungua ukilinganisha na miaka ya nyuma. Jitihada zetu kama TFS kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri tunaendelea kutoa elimu juu ya za uchomaji moto ovyo. Sambamba na hilo, tumeamua kugawa miche mingi ya miti ili wananchi wapande kwenye maeneo yao ili kupunguza kasi uchomaji wa moto bila kuwa na tahadhari. Kwa kugawa miche hii ya miti, kila mmoja atakuwa mlinzi wa mwenzake ili kuinusuru miti yake"
#RamadhanSaid
#MhifadhiMisitu (W) Ludewa.
"Mahitaji ya watu wanaohitaji kupanda miti kwa Wilaya ya Ludewa yameongezeka. Sisi Kama TFS kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Wilaya ya Ludewa tumejipanga kwa mwaka 2023/2024 kuzalisha miti mingi zaidi ukilinganisha na wakati huu ili kuongeza kasi ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa ujumla ikiwemo kuvinusuru na kuviimarisha vyanzo vya maji"
#RamadhanSaid
#MhifadhiMisitu (W) Ludewa.
"Tumepewa gari kwa ajili ya kutuwezesha kutoa elimu ya Uhifadhi pamoja na utunzaji wa mazingira kwa ujumla ikiwemo upandaji miti. Pia, gari hili litatusaidia kufika maeneo mengi zaidi na kwa haraka ili kuhakikisha rasilimali misitu na nyuki zinatunzwa kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijavyo".
#RamadhanSaid
#MhifadhiMisitu (W) Ludewa
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.