Wadau wa Kilimo nchini wamefika na kukutana na Wataalamu wa Kilimo wa Tarafa ya Liganga na Tarafa ya Masasi Wilayani Ludewa ambapo leo Ocktoba 03, 2022 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa vikao kazi na semina kwa wataalamu wa Kilimo wa maeneo hayo yaliyofikiwa na mradi wa CARE- myAgro Project.
Mradi wa CARE- myAgro umezifikia Tarafa mbili za Wilaya ya Ludewa kwa lengo la kuendeleza Kilimo cha mazao ya Alizeti, Karanga na Bamia
Pamoja na Uhamasishaji wa Kilimo cha mazao hayo Mradi huo umelenga kutokomeza Udumavu kwenye jamii yote ya Wilaya ya Ludewa kwa kuwafundisha wakulima kula chakula bora na kulima mbogamboga kwenye bustani za majumbani mwao.
Kikao hicho kitakuwa ni cha siku 2 ambapo mara baada ya kikao kazi kukamilika siku ya kesho Oktoba 04, 2022 waseminishaji hao watakwenda kwenye Tarafa hizo kuanzisha vitaru darasa kwa lengo la kuwafundisha wakulima kusimamia Mashamba yao kwa usahihi
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.