Jana Februari 15, 2023 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mheshimiwa Wise Mgina aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Castori Kibasa pamoja na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Ndg. Daniel Ngalupela kutembelea shule ya sekondari ya Lugarawa kwaajili ya kukagua na kupokea taarifa ya uunguaji wa bweni la wavulana katika shule ya sekondari Lugarawa.
Bweni la wavulana katika shule hiyo limeteketea kwa moto uliounguza zana mbalimbali za wanafunzi pamoja kuleta uharibifu wa bweni hilo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Februari 14, 2023 wakati wanafunzi wa bweni hilo wakiendelea na masomo ya usiku darasani.
Bweni limeungua na moto uliosababishwa na shoti ya umeme na kusababisha hasara ya kiasi cha shilingi milioni 18.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kusema kuwa, "Wanafunzi wanaoishi katika bweni hilo ni takribani 80 wa kidato cha kwanza hadi cha nne kwa tathimini ya haraka haraka ni karibu milioni 18 hivi za hasara zimeweza kutokea kwa maana ya kuwa kuna uharibifu wa miundombinu ya bweni hili kwa maana bati,mbao,vifaa pamoja na mavazi ya wanafunzi hawa,magodoro,mablangeti na mashuka" asema Kibasa.
Aidha aliongeza kwa kusema, hakuna mwanafunzi yeyote aliyepata madhara na badala yake wanaendelea na masomo kama kawaida huku serikali ikiangalia namna ya kulirejesha bweni hilo.
"Wanafunzi 57 vitu vyao vyote vimeteketea wamebaki na mavazi waliyovaa wakati huo wakiwa prepo. Kama Halmashauri tunahakikisha wanafunzi wanakuwa salama katika eneo la shule" alisema Kibasa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lugarawa Erasto Mhagama alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kwamba bweni linaungua, alifika na kushirikiana na wananchi kuuzina moto huo hadi walipofanikiwa kuuzima.
"Vitu vyote vimeungua moto, vitanda, magodoro, matraka na jitihada tulizochukua ni kuwashirikisha viongozi wa wilaya ili kutatua tatizo hili.Tukio hili ni la kwanza kutokea na kuleta uharibifu mkubwa" alisema Diwani Mhagama.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.