Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa Ndg. Stanley Kolimba Jana Machi 18, 2022 alizungumza na wananchi walio jitokeza katika hafla ya Miaka 10 ya shirika la PADECO walio jitokeza katika Kata ya Mundindi shule ya msingi ya watu wenye mahitaji maalum.
Ndg.Stanlye Kolimba alisema kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja wa uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amefanya mambo mengi ikiwemo Miradi ya Maendeleo ya Afya,Miradi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na Miundombinu ya Barabara. Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kuwa, tunakila sababu ya kumshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maendeleo anayo yaleta nchi kwetu haswa kwenye miradi inayo ishi, ikumbukwe kwamba Mwaka huu 2022 Mhe.Rais ametupati Fedha nyingi ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA pale Shaurimoyo ambapo ujenzi wake tayali umeanza na utarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Katika hatua nyingine Kolimba alisema Shirika la Padeco ni moja ya mashirika yanayo hitaji kuigwa haswa kwa kurudisha fadhira ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Wilbaard Mwinuka kwa kuendelea kuijenga Wilaya ya Ludewa kwa miradi ya kimaendeleo.
Nakupongeza kijana wetu kwa kuona umuhimu wa kuja kusaidia wototo hawa na kuwapa zawadi Bweni hili pamoja na vitanda,Magodoro 50 bado ukajenga na vyoo vitano na ukaongeza Usafiri wa pikipiki wa kuwahudimia pindi wanapo pata shida Hongera sana kijana,Sisi kama chama cha mapinduzi Wilaya ya Ludewa tunautambua Mchango wako kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,endelea hivyo hivyo na moyo wa upendo.
Wilaya yetu inafunguka kwa mambo mengi endelea kukaribisha wageni kutoka maeneo yote waje wawekeze kwenye Halmashauri yetu uchumi Utaongezeka.
Kwa upande wake Kaimu Katibu wa wazazi CCM Wilaya ya Ludewa Ndg. Salum Mohamed Mfaume alisema kuwa uwepo wa bweni hilo ambalo Shirika la PADECO limeiwezesha shule hiyo itawafanya watoto wanao soma hapo kuishi vizuri na furaha wakiyafurahia mazingira hayo, aliendelea kusema kusema kuwa watoto ni Taifa la kesho hivyo kila mtoto aliye zaliwa anahaki ya kupata elimu kwa kauli mbiu isemayo, Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.