Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva akiambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Mbunge wa Jimbo la Ludewa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja naWakuu wa Divisheni Jana tarehe 25 Aprili 2023 walipokea Mwenge wa Uhuru 2023 uliowasili wilayani Ludewa na kuanza kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zimeongozwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim, kwa mwaka 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilikuwa na miradi 8 yenye thamani ya bilioni 2.24 imekaguliwa na kufunguliwa.
Sambamba na hayo Mwenge wa Uhuru 2023 unaongozwa na kaulimbiu isemayo, “MABADILIKO YA TABIA NCHI, HIFADHI MAZINGIRA NA UTUNZAJI WA
VYANZO VYA MAJI.” TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWAUSTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA.”
Wilaya ya Ludewa kwa kipindi cha mwaka 2023 imepanga kupanda miti 7,000,000 na hadi sasa wilaya ya Ludewa imefanikiwa kupanda miti 5,250,000 ambayo ni sawa na asilimia 75 ya lengo. Aidha kazi ya upandaji bado inaendelea.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.